GET /api/v0.1/hansard/entries/524930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 524930,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/524930/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Mwisho kabisa nataka kuunga mkono Mswada huu kwa sababu umekuja kwa wakati mwafaka. Tumeona mambo mengi kama ya Anglo Leasing, Goldenberg na mengine ambayo yalitokea, lakini kwa vile hakukuwa na kitengo ambacho kilikuwa kimethabitiwa vizuri, tunaona ni mazungumzo yamezungumzwa halafu baadaye rasilimali ya wananchi ikapotea katika mikono ya watu wengine. Kwa hivyo, bodi ikiwako pamoja na ofisi hii nina hakika zitaweza kuchukua hatua ambayo itaweza kulinda rasilimali zetu sisi kama wananchi wa Kenya. Kwa hivyo ninaunga mkono Mswada huu na kusema kuwa ni muhimu tuweze kuupitisha. Ahsante."
}