GET /api/v0.1/hansard/entries/526190/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 526190,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/526190/?format=api",
"text_counter": 22,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Spika, wingu la mauti limetanda tena kulifunika Bunge hili. Kumpoteza mmoja wetu wa Bunge la Kitaifa sio jambo la furaha. Siwezi kujitapa kwamba nilimfahamu kwa utu marehemu lakini alijulikana Kenya nzima kwa utekelezaji wake wa kazi hasa akiwa kiongozi kwa vyama vya wafanyikazi. Alikuwa mcheshi na mtu mwenye busara. Umri wa miaka 66 ni umri wa mtu aliyekomaa, asiyeogopa na aliyefika wakati wa kuwaongoza watu na kuwapa ushauri akiwa bado na nguvu kwa uzee wake. Tumepokonywa kiongozi huyu akiwa na askari wawili wamemzunguka wakiwa na bunduki mbili, yeye mwenyewe akiwa na bunduki. La ajabu ni kwamba muuaji aliwapiga risasi moja kwa moja bila hata risasi moja kutupwa kujikinga. Jameni, ingekuwa ni jambo la hirizi, tungezitupa. Lakini ni maajabu kwamba jambo lile limetendeka akiwa na askari wawili ambao tunaamini kwamba walikuwa wamepate mafunzo ya kutosha kwa kazi yao ya uaskari. Lakini ni kudura ya Mungu kwamba haya huwezi kuyasema, kifo chako kikifika, kimefika. Juzi, Kamati ya Usalama na Maswala ya Kigeni ya Bunge la Kitaifa ilisema kwamba inataka muuaji atajwe kwa masaa kadhaa. Kama wanamjua, kwa nini wasimtaje? Wamtaje badala ya kupoteza muda wakingoja atajwe na wengine. Vile The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}