GET /api/v0.1/hansard/entries/526214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 526214,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/526214/?format=api",
"text_counter": 46,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kenya, tunaahidiwa kwamba “hakuna jiwe ambalo halitapinduliwa.” Lakini wakati Tom Mboya alikufa, hakuna jiwe ambalo lilipinduliwa. Pia, wakati Dkt. Robert Ouko, JM Kariuki na wengine walikufa, hakuna jiwe ambalo lilipinduliwa. Jambo la kushangaza ni kwamba, mambo yaliyotokea mwanzo yalionyesha kwamba Mheshimiwa George Muchai aliuwawa na mtu mmoja ambaye alikuwa amefunika uso wake ingawa alikuwa na wenzake. Baada ya kumuua Mhe. Muchai, mtu huyo aliingia kwa gari lao na hatimaye wakaondoka. Ninataka kueleza Serikali ya Jubilee na wale ambao wanasimamia vitengo vya usalama kwamba sisi, Wakenya, tunaangalia na tumefungua masikio kusikiliza. Hii ni kwa sababu haitawezekana tuambiwe kwamba walioteka nyara wanawake wawili, waliwapeleka kwa benki kutoa pesa katika ATM, na ni wao hao ambao wanaonekana wakipeleka watu kutoa pesa katika ATM na usiku wa manane haujaingia, ana mwanamke amefungwa mikono na hakuna mtu mmoja, hata askari, anaweza kusema: “Nimeona watu wakipita hapa, walikuwa na mwanamke aliyefungwa mikono, na amepelekwa katika ATM kutoa pesa.” Anashindikizwa kutoa pesa, anafungwa tena na kuwekwa katika buti ya gari. Halafu wakiwa pale, akiwa katika buti, anasikia risasi ikilia na anajua kwamba ni George Muchai ameuawa. Kama wako na tabia hiyo na sio pesa, kwa nini wasiwaue wale wanawake wawili kwanza? Wanawabeba kwa gari, wanakuta gari la mtu ambaye hawamjui, wanatoka, wanafyatua risasi na kuua kila mtu ndani ya gari na tena wanarudi katika lile lile gari, wanaondoka na wanawake wale na hakuna mmoja aliyepata madhara. Sisi tunatoa kodi na tunaajiri askari watufanyie kazi. Tunataka kujua ni nani alimuua George Muchai na hatutaacha mpaka tuelezwe ukweli. Natuma rambirambi, Bw. Spika."
}