GET /api/v0.1/hansard/entries/526605/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 526605,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/526605/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Spika. Kwa niaba ya watu wa Mvita, ningetaka kuchukua fursa hii kutoa pole na risala za rambirambi kwa familia ya Mhe. Muchai pamoja na wale askari na dereva wake. Kuna kitu ambacho ningependa kutaja. Wenzetu ambao wameinuka wamesema kuwa kuna haja ya askari wa Wabunge kuongezwa na kupatiwa vifaa zaidi. Lakini kando na kujifikiria na kutufikiria sisi, tunafaa kuchua fursa na kuweka mbele maswala mawili. La kwanza, ni kuuliza ikiwa zile kamera ambazo zimetumia thamani kubwa ya pesa za wakenya zimetumika kwa njia inayofaa. La pili, ni lazima sisi kama Wabunge tukubaliane na tuhakikishe tumepitisha Miswada kuhakikisha kuwa kila askari ambaye atakufa akiwa kazini, awe anamlinda Mbunge au mtu yeyote mwingine, fidia ilipwe familia yake ili iweze kuendelea baada ya kifo cha huyo askari. Langu ni kutoa risala hizo za rambirambi na kuiuliza familia yake iwe na subira katika wakati huu wa huzuni."
}