GET /api/v0.1/hansard/entries/526623/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 526623,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/526623/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Thank you very much, hon. Speaker. Kwa niaba ya wananchi wa Kwale, ningependa kuchukua fursa hii nitoe rambirambi zangu na zao kwa familia ya marehemu Muchai, familia ya walinzi wake pamoja na familia ya dereva wake. Tukiwa tunaomboleza kifo cha mwenzetu, wakati umefika sisi kama Wakenya - nikisema sisi kama Wabunge tutakuwa tumejitenga, tungependa tujue. Tulimwona Rais wa nchi yetu akianzisha ule mradi wa kamera ambazo zinamulika mienendo yote katika eneo la Nairobi. Kamera hizi kweli zafanya kazi, ama wale ambao wanapaswa kuwa wanazisimamia walikuwa wamelala? Hii ni kwa sababu mahali ambapo aliuliwa mwenzetu ni katikati ya mji na katikati ya hizo kamera. Tunataka kujua wale wanaohusika walikuwa wapi, na kama walikuwa wako macho waliona nini. Wakenya wanataka kujua kitu gani kilitokea mpaka mauti ikamfika mwenzetu. Nikirudi upande wetu sisi Wabunge, naomba kwa unyenyekevu tuweze kuwa na muda ambao tutakuwa tukiwaachia wale maaskari wetu nafasi ya kuweza kulala na wapumzike ili wakati wanapotulinda waweze kuwa na nguvu na kuwa macho. Hebu angalieni wakati wale vijana walikutana na mauti. Ni wakati ambao kusema ukweli ilikuwa inapaswa kuwa pengine wanapumzika nyumbani kwao na familia zao. Pia hata sisi wenyewe---"
}