GET /api/v0.1/hansard/entries/526646/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 526646,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/526646/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1022,
        "legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
        "slug": "joyce-wanjalah-lay"
    },
    "content": "Asante sana mhe Spika. Ninataka kuungana na wenzangu kutoka Kaunti ya Taita Taveta kutoa rambirambi zetu. Kwa kweli ni jambo la kuhuzunisha sana. Kama vile Wabunge wametangulia kusema, ni muhimu kwa wanaotulinda, na wanaolinda Kenya kwa ujumla, wapate mafundisho mara kwa mara. Vile vile, ninataka kueleza Bunge hili kwamba Wakenya wamechoka kusikia kwamba uchunguzi utafanywa na hakuna jiwe litaachwa bila kupinduliwa. Tumechoka kusikia kwamba ukweli utapatikana na haupatikani. Jambo hili husemwa kila wakati na hatuambiwi ukweli. Hatuambiwi ni nani ameshikwa na ni nani amefanya kitendo kama hiki. Kama mkenya ametoa ripoti kwamba maisha yake yamo hatarini, mbona uchunguzi usianzie hapo? Usalama unazingatiwa baada ya mtu kufariki. Kama nimeripoti kwamba maisha yangu yamo hatarini, wale wanaoshugulika na mambo ya usalama wanafaa kuanza uchunguzi na kuwashika wanaopanga njama za kuuwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}