GET /api/v0.1/hansard/entries/526677/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 526677,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/526677/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "wake, kulikuwa na tatizo. Naomba kwa unyenyekevu Wabunge wenzangu tuangalie kwa ufasaha sana shughuli za Bunge na mikakati yote ambayo itawekwa mbele ya Bunge hili. Ni hii kamati peke yake ambayo ina majukumu ya kuweza kufuatilia na kuongoza shughuli za Bunge. Kama ilivyosemwa na kiongozi wa walio wengi Bungeni, tusipoikubali hii Hoja leo, inamaanisha kuwa Bunge kesho halitakuwa na ratiba yoyote ambayo itaweza kufuatwa, na Bunge halitaweza kufanya shughuli zake. Kwa hivyo, nasihi pande zote za milengo ya kisiasa tuungane, tushikane pamoja tuanze muhula huu mpya kwa moyo wa kuridhiana na kwenda mbele ili tupate kuijenga hii nchi. Majina ambayo yako hapa, yametoka kwa milengo yote. Labda kuna wengine ambao walikuwa wanatarajia kuwa katika hii kamati lakini hawakuweza kubahatika. Ukweli wa mambo ni kuwa si kila mtu ataweza kuwa katika hii kamati kwa sababu idadi yake haiwezi kuwa zaidi ya watu 29, kama ambavyo imekubaliwa na kanuni za Bunge. Kwa hivyo, nawaomba Wabunge wenzangu tushikane, tuweke maanani na tujue kuwa hawa wote ambao wamechaguliwa, ama kuteuliwa, watakuwa kama nyinyi wenyewe wa milengo yote. Tuhakikishe kuwa shughuli za Bunge zinafanikiwa. Naomba vilevile katika uendeshaji wa shughuli zetu za Bunge muhula huu, tukiona kuna Hoja ambayo inaleta utata, ama italeta utata, tukae kando kidogo, hasa viongozi, tujadiliane na tuipige msasa ili inapoletwa hapa isije ikapendelea mlengo wowote, na kuleta fujo. Tunaomba tuelekee pamoja. Tushikane twende kama dau moja. Tushikane ili ile hadhi yetu ambayo imeshushwa sana na mikasa ambayo ilitokea hapo awali, hasa mwisho wa muhula, irudi na kupanda. Nikimaliza, naomba nichukue hii nafasi kama mmoja wa Wabunge na, kwa niaba yangu na ya watu wa Wundanyi ambao ninawakilisha kupeana rambirambi zangu na zao kwa familia ya mhe ambaye amepatwa na mkasa wa kifo, labda kabla ya wakati wake kufika. Mauti yalimfika familia yake ikiwa inaangalia. Tukiangalia katika utu wa binadamu, mtu kulimbikiziwa risasi watu wakiangalia--- Walinzi wake na driva walikuwa watu wachanga walipokufa. Ni kifo ambacho mpaka sasa sisi, kama Wabunge, hatujaelezwa waziwazi kilitendeka vipi. Vifo vingine vimetokea na tunavielewa. Lakini hiki cha mwenzetu, mhe Muchai, tunaomba mkono mrefu wa Serikali uingilie kati na uchambue kwa undani ili tufahamishwe ni nini kiliwafanya wenzetu kutuacha. Kwa hivyo, natoa rambirambi zangu kwa wote ambao wanahusika, familia, jamii na marafiki zake. Wabunge wenzangu pia nawapatia pole kwa kupoteza mwenzetu. Mwenzetu mwingine ametoa Hoja hapa na kusema pia amepata vitisho; tusivichukulie rahisi namna hio. Hii ni kwa maana kama mwenzetu anapata vitisho, hatujui ni nani mwingine atapata vitisho. Naomba ulinzi wa Wabunge upewe kipaumble ili sote tupate kuhakikishiwe kuwa tukitoka hapa na kwenda kwa shughuli mbali mbali tujue tuko katika hali nzuri ya ulinzi. Narudia kuwasihi Wabunge wenzangu wa pande zote tuunge mkono hii Hoja, na labda tusiizungumzie kwa urefu sana lakini tuipitishe. Naunga mkono."
}