GET /api/v0.1/hansard/entries/529556/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 529556,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/529556/?format=api",
"text_counter": 245,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ni mmoja wao. Tuna Waislamu na Wakristu ambao wanaomba kabisa. Kusema kweli, tumeyaona mengi yakifanyika katika nchi hii. Haya yote yameunganisha taifa hili kabisa tukawa kitu kimoja. Tumeona ushindi mkubwa katika taifa hili. Nikiangalia, naona ICC ilikuwa ilete udhaifu mkubwa lakini kupitia maombi, hayo yote yameshindwa. Kupitia maombi, tumeona Rais na Naibu wake walichaguliwa na Wakenya wote waliona. Kwa hayo yote, namshukuru Mwenyezi Mungu. Ningependa kuomba tuzidi kuweka maombi mbele kama taifa. Tuliona vile Rais wetu alijishusha, tuliona vile naibu wake alijishusha. Baada ya kupewa madaraka, aliyashikilia bila mchezo. Aliyashikilia vizuri mpaka Rais akarudi. Viongozi wetu wametuonyesha kwamba wao ni mashujaa na wazalendo wa nchi hii. Wametuonyesha kwamba miaka mingine itakapokuja, hatutaangalia nyuma. Tutawachagua wale wale tu, 2017. Hata baada ya mwaka huo, tutachagua naibu wake. Tumeona hayo. Bwana Omar Hassan ni rafiki yangu. Hata yeye alijionea kwamba uzalendo ulitumika pale."
}