GET /api/v0.1/hansard/entries/529592/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 529592,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/529592/?format=api",
"text_counter": 281,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Njoroge",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13158,
"legal_name": "Ben Njoroge",
"slug": "ben-njoroge"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Hoja iliyoko mbele ya Seneti. Kwanza, napenda kuunga mkono Hotuba ya Rais iliyotolewa tarehe sita Oktoba. Rais alionyesha ujasiri mkuu na heshima yake kwa Bunge letu – lile la Kitaifa na pia Bunge la Seneti. Bw. Spika, ujasiri ulioonyeshwa na viongozi wetu, haswa Rais wetu, kwa kukubali kuelekea kule The Hague kuhudhuria kesi katika mahakama ya ICC ilikuwa jambo la busara sana. Lakini hata wakati ninapofikiria kuondoa siasa katika ile korti kuhusiana na mashtaka yanayomkabili Rais, pia ninashawishiwa na lile korti ama kiongozi wa mashtaka alipokuwa anaendelea kutoa ombi lake kwa majaji ili waweze kuahirisha ile kesi inayomhusu Rais. Bw. Naibu Spika, nakumbuka wakati mmoja ambapo kiongozi wa mashtaka aliwaeleza majaji wapeane muda kwa sababu mwaka wa 2017 unakuja na kutakuwa na uchaguzi hapa Kenya. Kwa hivyo, upande wa mashtaka ni kama ulikuwa unaahidi kwamba tukiingia katika uchaguzi wa mwaka 2017, Rais asipochaguliwa tena, pengine watapata ushahidi waliokuwa wakitarajia. Upande wa The Hague ulijaribu kushawisha majaji kwamba jambo hili linahusishwa na siasa. Licha ya hayo, niliona kwamba upande wa mashtaka umeahidiwa na watu fulani kwamba Rais akiondoka katika mamlaka, watapeana ushahidi katika The Hague. Walijaribu kuwasawisha majaji ili wakubali kuhahirisha kesi wakitarajia kwamba uchaguzi ukija katika mwaka wa 2017, kutakuwa na kiongozi tofauti na si Rais Uhuru Muigai Kenyatta. Bw. Spika wa Muda, viongozi wameonyesha ujasiri mwingi ambao ni wa hali ya juu. Pia, ningependa kuwaunga mkono. Kama vile tumesikia mali ya Seneta mmoja ya dhamana ya Kshs25 milioni iliharibiwa huko Migori. Ningependa kujiuliza kama mambo hayo yalifanywa na Rais na Naibu wake. Ni Rais na Naibu wake ambao walienda Migori The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}