GET /api/v0.1/hansard/entries/529594/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 529594,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/529594/?format=api",
    "text_counter": 283,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kuharibu mali? Tumesikia kwamba huko Kisumu na kwingineko kama Mombasa kulikuwa na ghasia. Vile ninavyoona, jambo hili lilienda kisiasa. Nashangaa kwa sababu wale waliofanya kitendo hicho hawakushatakiwa. Wao walibaki wapi wengine walipokuwa wakishtakiwa? Mimi kama mkaaji wa Naivasha, sehemu moja ambayo Rais anatajwa kuhusika nilishangaa kwa sababu hakuna wakati Rais alikuja Naivasha. Ni jambo la kusikitisha wakati Rais anatajwa katika mambo ambayo hayawezi kuthibitishwa kortini. Licha ya hayo, ni jambo la kushangaza na kilio kilichokuwa katika upande wa mashtaka. Walikuwa wakitaka kujua kama mshtakiwa angewasaidia na ushahidi. Hilo ni jambo ambalo katika sheria halikubaliwi. Mtu hawezi kumshtaki mtu, bila ushahidi halafu kuanza kumtisha mshtakiwa kutoa ushahidi ili aweze kuendelea na mashtaka. Hilo ni jambo la kushangaza sana. Ninaamini pia viongozi wetu ni wacha Mungu. Hiyo ndio sababu wale ambao wamewashtaki hawana ushahidi. Ni jambo la kufehedhesha kusikia kwamba kiongozi wa Mashitaka alishawishi majaji ambao walikuwa wakisikiliza kesi kwamba katika mwaka wa 2017, watapata ushahidi ambao watakuwa wakitaka. Wale tuliokuwa katika korti tulishangaa ni nani atakuwa kiongozi katika nchi hii. Watu wengine katika mrengo wa upinzani ambao walikuwa wakitaka Rais aende koti la The Hague walitarajia kwamba hangerudi. Walishangaa sana waliposikia kwamba Rais angerudi Kenya bila shida yoyote. Kwa hivyo, wale ambao walikuwa wa kwanza kusema aende The Hague, tunajua wazi hawakuwa na nia nzuri. Walikuwa wakidhani kwamba Rais Uhuru hangerudi nchini. Ningependa kumpongeza Makamu wa Rais ambaye alipowachiwa mamlaka kwa kuongoza nchi hii kwa masaa 48. Alionyesha ujasiri na ungwana kwa kumrejeshea Rais kiti chake aliporudi nchini. Wakati Rais alipofika huko Netherlands, Wakenya walimuonaje akiingia huko kama raia. Hili ni jambo ambalo litakuwa funzo kwa Wakenya wote. Utakumbuka pale mwanzo ambapo bahasha ilienda na Bw. Kofi Anan. Wakenya walimruhusu yeye kwenda na hii bahasha hata kama hatukujua ilikuwa na majina ya akina nani. Wale ambao walimsawishi Rais kukubali bahasha kutoka Kenya bila kukaguliwa kilichokuwa ndani walifanya makosa. Kulikuwa na dosari hapo. Mambo ambayo tunayaona sasa si mazuri. Kiongozi kupelekwa mpaka The Hague bila ushahidi ni jambo la aibu. Hili ni jambo ambalo hatungekuwa nalo wakati huu kama bahasha hiyo haingetoka nchini bila kukaguliwa na kuona uongo uliokuwa ndani. Tumesikia wengine wakisema vile walihongwa na vile waliahidiwa mambo makubwa ili watoe ushahidi wa uongo. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Hotuba hii."
}