GET /api/v0.1/hansard/entries/530748/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530748,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530748/?format=api",
"text_counter": 35,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "Hoja hii pekee isisaidie.Ni muhimu tubadilishe sheria kwa kuweka hatua za kinidhamu na kuhakikisha kuwa watu wametii sheria hiyo. Ni kweli kuwa NACADA haijaweza kufikia kila sehemu ya nchi. Kwa hivyo, mambo ya ulevi na upikaji wa pombe haramu bado unaendelea. Watu wengi siku hizi wanaokota chupa za kuweka pombe. Wanaweka chochote ambacho wanataka hata kama ni chang’aa ambayo imepikwa kando ya mto katika njia chafu. Wengine wao huongeza kemikali kwenye pombe hiyo. Wateja hudanganywa kuwa wanachonunua ni pombe ambayo wamezoea. Kule River Road na eneo la Gikomba kunazo nyumba ambazo hutumika kuweke kemikali katika chupa za pombe. Nakubaliana na mhe. Njenga kuwa hatua inastahili kuchukuliwa kwa watu kama hao. Nitashirikiana naye na nitauunga mkono Mswada utakaoletwa wa kusaidia hali hii mbaya. Hii ni Hoja nzuri na tunaomba Serikali ichukue hatua. Sisi kama watunga sheria twastahili kupandisha hii Hoja hadhi ili iwe Mswada. Tukifanya hivyo, tutalishughulikia jambo hili vema. Ukiongea na wataalamu katika hii sekta ya pombe, watakuambia kwamba hii nchi inapoteza pesa nyingi sana kwa magonjwa yale ambayo inatubidi kutibu kwa sababu ya ulevi. Shule nyingi zinakuwa na migomo kwa sababu ya wanafunzi kunywa pombe. Walimu na wataalamu wengine humu nchini wameathirika kwa ajili ya pombe haramu. Hii imeathiri uchumi wa nchi yetu. Ni ombi langu kuwa huo Mswada uletwe hapa haraka iwezekanavyo. Ningemsihi mhe. Njenga na wahusika wengine waangalie zile sheria zinazohusiana na suala la pombe. Ningependa mhe. Njenga apanue hii Hoja yake ili iweze kubadilisha sheria hizo zote ndiposa tuweze kushughulikia yale ambayo yamelengwa na hii Hoja. Ninaunga mkono."
}