GET /api/v0.1/hansard/entries/530817/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530817,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530817/?format=api",
    "text_counter": 104,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "mhe Naibu Spika, ukiviangalia hivi vipengele katika Katiba yetu, utaona kwamba sisi kama Wakenya tumekubali kwamba lugha ya Kiswahili ndiyo lugha ya kitaifa. Hiyo ni kumaanisha kwamba lugha hii ina maana zaidi kushinda hata lugha ya Kiingereza, ambayo imetujia sisi kutokana na historia yetu – tulikuwa koloni la Uingereza. Jambo la kushangaza ni kwamba lugha ya Kiswahili bado haijatiliwa maanani kama inavyopaswa. Ndiposa namshukuru mhe Lay kwa kufikiria jinsi hii."
}