GET /api/v0.1/hansard/entries/530818/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530818,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530818/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Tukianzia hapa kwetu Bungeni, kanuni za Bunge haziko katika lugha ya Kiswahili. Kamati ya Kanuni, Itifaki na Mienendo ya Bunge inafaa kuangazia umuhimu wa kutafsiriwa kwa kanuni za Bunge kwa lugha ya Kiswahili. Mhe Lay amethibitisha kwamba unapotunga Hoja na Miswada kwa madhumuni ya kuileta Bungeni, ni lazima uandike kwa lugha ya Kiingereza. Hilo ni jambo la kufedheesha. Mimi mwenyewe nimejaribu kubuni Hoja kwa lugha ya Kiswahili lakini maafisa wa Bunge wanaopaswa kutusaidia kufanya hivyo, hawaielewi lugha ya Kiswahili. Hili ni jambo ambalo tunapaswa kuliangazia ili tuweze kuwa na wafasiri ambao wanaweza kutusaidia sisi Wabunge kujieleza rasmi katika Bunge hili."
}