GET /api/v0.1/hansard/entries/530820/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530820,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530820/?format=api",
"text_counter": 107,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Kiswahili ni lugha ambayo ina mashiko makuu sana katika historia ya Kenya. Kiswahili ni lugha ya kiafrika. Wengi watakubaliana nami kwamba Kiswahili kimetiririka kutoka kwa lugha za kiafrika. Ukitembea katika nchi nyingi za kiafrika utapata maneno mengi ambayo yanawiana na lugha yetu ya Kiswahili. Kwa mfano, lugha ya Kizulu kule Afrika Kusini, lugha za kizambia kule Zambia na hata humu nchini, zinawiana na Kiswahili. Mimi mwenyewe, nikiiangazia lugha yangu asilia, kuna maneno mengi sana ambayo yanawiana na Kiswahili. Sembuse kusema kwamba jina “Swahili” limetokana na jina la kiarabu ‘sawahil’ – watu ambao wanaishi katika ufuo wa bahari."
}