GET /api/v0.1/hansard/entries/530821/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530821,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530821/?format=api",
"text_counter": 108,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Jambo muhimu ni kwamba ukiitizama lugha hii, utaona kwamba haina watu ambao unaweza kusema haswa ndio watu ambao wanaweza kuienzi kama lugha zingine za Kikuyu, Kiluo, Kiluhya na kadhalika. Kwa hivyo, ni lugha ambayo inaweza kutujumuisha sisi kama Wakenya bila ya watu wengine kuhisi kwamba wao, kwa sababu ya lugha hii, wako sawa zaidi kuliko watu wengine. Ukiangazia changamoto ambayo sisi kama Wakenya na pengine watu ambao wametumia lugha za kigeni kama lugha zao za kitaifa, ni kwamba kunakua na kukanganya kidogo wakati dhana zako ziko katika lugha ile halafu wewe mwenyewe unajieleza katika lugha yako ya Kiswahili. Mara nyingi, watu wanakataa kuzungumza Kiswahili hususa kwa sababu za kilahaja. Hakuna shule yoyote ambako watu hufundishwa lahaja ama lafudhi. Ni muhimu Wakenya tuelewe kwamba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}