GET /api/v0.1/hansard/entries/530823/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530823,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530823/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Mhe Naibu Spika, lahaja ya Kiswahili tunayotumia ni ya kizanzibari. Kuna lahaja nyingine za Kiswahili kama vile Kimvita, Kimtang’ata, Kipemba na kadhalika. Hata kule pwani, lugha ya Kiswahili ambayo inazungumzwa kule Mombasa ni tofauti sana na lahaja ya Kiamu, ambayo inatumika kule Lamu. Kwa hivyo, hii njia ni ya kuweza kusema kwamba watu hawawezi kujieleza kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu katika kufundisha lugha hii kule shule, kuna mtazamo wa kuisanifisha lugha – mtazamo ambao unawafanya watu kuhisi kwamba hawawezi kuizungumzia lugha hii kwa misamiati. Kwa hivyo wanaogopa. Lakini la hasha! Ninaikataa dhana hiyo. Mara nyingi sisi, kama wanasiasa, tunapoenda mashinani tusiwe tukizungumzia wananchi wetu kwa Kiingereza. Mara nyingi tunazungumza kwa lugha ya Kiswahili. Kiwe Kiswahili sambamba ama Kiswahili kombokombo, la muhimu ni kwamba Wakenya wengi wanaweza kutuelewa vilivyo wakati tunazungumza katika lugha ya Kiswahili. Mhe. Naibu Spika, hili ni jambo ambalo kama tunaweza kuitumia lugha hii, tunaweza kuzifungua fikra na dhana za watu wengi. Watu wengi hawawezi kuzungumza kwa lugha ya Kiingereza kwa ufasaha. Kwa hivyo, wanaogopa kujieleza kwa lugha ya Kiingereza. Wanaonekana kama ni wajinga ilhali ukiwasikiza katika lugha za mama na katika Kiswahili, wana Hoja nzuri na wanaweza kuchangia katika maendeleo, hususan ukiangazia kwamba watu wetu wengi hawajasoma vilivyo na ni wa kipato cha chini na hawajaweza kuwa na ule upana wa kujua vile mambo yanaweza kuendeshwa katika nyanja tofauti tofauti."
}