GET /api/v0.1/hansard/entries/530841/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530841,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530841/?format=api",
    "text_counter": 128,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Ninayo masikitiko makubwa kwa sababu Katiba ya Kenya haijatafsiriwa rasmi katika lugha ya Kiswahili; Katiba bado ni rasimu. Kipengele sabini na saba katika Kanuni za Bunge kinatambua Kiswahili kama lugha rasmi ya Kenya. Kipengele cha saba katika Katiba kinatambua kwamba Kiswahili ni lugha rasmi na tena lugha ya taifa. Iwapo Kiswahili ni lugha rasmi na tena lugha ya taifa, kwa nini Katiba hiyo haina tafsiri rasmi ya Kiswahili? Kwa sababu hiyo, mimi namshukuru mheshimiwa Mbadi kwa kuleta marekebisho haya. Nilipoongea mara ya kwanza katika Bunge hili la Kumi na Moja, hatua ya kwanza niliyochukua ilikuwa ni kupendekeza na kuandikia Kamati ya Bunge inayohusika na Kanuni za Bunge. Kwa bahati mbaya mpaka leo sijapata jawabu. Nimeomba Kamati ya Kanuni ya Bunge itafsiri Kanuni za Bunge kwa lugha ya Kiswahili. Tangu 2013 hadi leo, Kamati hiyo haijaweza kunipa jawabu kama inaweza kutafsiri Kanuni za Bunge ama la. Ninasikitika sana. Kwa hivyo ninaunga mkono waheshimiwa Mbadi na Lay. Mimi ninaamini kwamba taifa letu litapata uhuru kamili siku ambayo mahakama itasikiza mashtaka kwa lugha ya Kiswahili na hakimu atoe hukumu kwa lugha ya Kiswahili ndiposa mshtakiwa aweze kujitetea. Tunajigamba eti tumepata Uhuru ilhali Wachina wanatufungia hoteli hapa. Kwa nini? Ni kwa sababu tunaiga mavazi yao na lugha zao. Heshima na uhuru wetu ni mambo ambayo hayatotambulika. Kwa hayo machache, nimesimama kuunga mkono marekebisho yaliyoletwa na ndugu yangu mheshimiwa Mbadi ili Katiba itafsiriwe rasmi katika lugha ya Kiswahili. Asante Naibu Spika wa Muda."
}