GET /api/v0.1/hansard/entries/530863/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530863,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530863/?format=api",
    "text_counter": 150,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Murungi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2802,
        "legal_name": "Kathuri Murungi",
        "slug": "kathuri-murungi"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Joyce Lay. Kwanza kabisa, naiunga mkono Hoja hii ikiwa na marekebisho ambayo yameletwa na Mhe. Mbadi. Katiba ya Kenya inasema kuwa tuko na lugha mbili za kitaifa ikiwa ni Kiswahili na Kiingereza. Sheria zote ambazo zimepitishwa Kenya hii zinafaa kutafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili ndio kila Mkenya azielewe. Katiba yetu inawapa Wakenya wote uhuru wa kupata habari na kujua chochote kinachoendelea. Lakini inaonekana kuwa wanaotunga sheria nchini wanawadhulumu wananchi. Ukienda kwenye korti zetu, mawakili hawapendi kuitumia lugha ya Kiswahili. Ni kama hawaelewi lugha ya Kiswahili vizuri. Kwa hivyo, wanapowatetea wafungwa, wanaitumia lugha ya Kiingereza ambayo ni ngumu. Hii inaonyesha kuwa Wakenya wanaumia na hawaongei. Hata sisi katika Bunge hili la Taifa, Seneti na bunge za kaunti, Wabunge wanafaa kupewa motisha zaidi ili waweze kuongea Kiswahili katika Bunge na kuleta Hoja kwa lugha ya Kiswahili. Nimeona Mhe. Mbadi ameshindwa kuzungumza Kiswahili akiileta Hoja yake. Ninaomba kila Mbunge ambaye analeta Hoja ama Mswada hapa, ajieleze kwa Kiswahili. Katika Hoja hii, tunajadili vile ambavyo tutaongea kwa Kiswahili katika Bunge hili na tutafsiri sheria kwa Kiswahili, lakini wenzangu wanaongea katika lugha ya Kiingereza. Tukae kama ndugu zetu Watanzania. Katika Bunge lao, hata yule profesa wa Kiingereza ambaye yuko pale, asilimia 90 ya wakati anaongea, anatumia lugha ya Kiswahili. Hawatumia Kiingereza katika Bunge lao. Watu wetu wote wanafaa kuelewa sheria ambazo tunatunga hapa Bungeni. Ninaiunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Joyce Lay. Wakati tunapotunga sheria hapa Bungeni, tunaweka kwa magazeti kuwa ni lazima wananchi washirikishwe katika utunzi huu. Hata tukiweka kwa magazeti, hatuweki kwa Gazeti la"
}