GET /api/v0.1/hansard/entries/530865/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530865,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530865/?format=api",
"text_counter": 152,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Murungi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2802,
"legal_name": "Kathuri Murungi",
"slug": "kathuri-murungi"
},
"content": "ambalo linatumika hapa nchini. Viongozi wa Bunge wanaweka ilani hizi kwa lugha ya Kiingereza kwa magazeti za Daily Nation na The Standard. Ningeomba tuanze hapa Bungeni wakati tunapowashirikisha wananchi katika kutunga sheria. Tunafaa kuweka ilani zetu na mambo ambayo tunafanya hapa Bungeni kwa lugha ya Kiswahili katika Gazeti la Taifa Leo . Hii itawashirikisha wananchi wote. Ninafahamu kuwa watu wengi wamefungwa kwa makosa ambayo si yao. Watu wengi wameenda kortini na hawakuelewa vile kesi zao zinaendelezwa. Wakielezwa kuwa Katiba inawapa uhuru fulani, hawajui inapatikana kwa kipengele kipi katika Katiba yetu. Nitawaomba mawakili, kwa sababu hapa tuko na mawakili wengi, wazungumze na wengine katika chama chao cha mawakili watakapomaliza vurugu zao, wawaambie kuwa wakienda kortini, waitumie lugha ya Kiswahili ndio wananchi wetu waelewe. Ninaona kuwa wenzangu wengi wana hamu na ghamu ya kuiunga nkono Hoja hii, ninaomba kumaliza. Ninaiunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na mbunge wa Taita Taveta, Mhe. Joyce Lay."
}