GET /api/v0.1/hansard/entries/530867/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530867,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530867/?format=api",
    "text_counter": 154,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Amolo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 631,
        "legal_name": "Rachel Ameso Amolo",
        "slug": "rachel-ameso-amolo"
    },
    "content": "Kwa kweli, litakuwa jambo la maana kabisa kama lugha ya Kiswahili itaenea kote kote katika nchi yetu ya Kenya. Tunapoingia shuleni, tunaanza kusoma Kiingereza na Kiswahili na tunaendelea vizuri. Lakini tukifika mahali fulani, hatuelewi kabisa Kiswahili kinapotelea wapi. Ukifika pale mbele katika ofisi zetu, hauoni tena Kiswahili. Tunaendelea kuongea lugha ya Kiingereza. Kwa kweli, kuna mambo mengi sana ambayo tunaweza kufanya tukitumia lugha yetu ya Kiswahili. Hasa tukiangalia zile kandarasi ambazo kina mama, vijana na wale hawajiwezi wanapewa, ziko katika lugha ya Kiingereza. Unashindwa kabisa kuwa wale ambao hawaelewi Kiingereza, watatumia lugha gani ili waweze kuzipata zile kandarasi. Bali na zile sheria kutafsiriwa kwa Kiswahili, mambo mengi katika nchi yetu yanafaa kufanywa kwa Kiswahili. Kama mambo fulani yameelezwa ka Kiingereza, chini yake yawe yameelezewa kwa Kiswahili. Kwa mfano, kama kuna ilani ya “toilets”, pale chini kuwe na maelezo ya “vyoo”. Hii itasaidia watu kuelewa. Kama ni barabara ambayo imeelezwa ka Kiswahili, inafaa kuelezewa pia kwa Kiswahili. Kwa hivyo, tusiangalie sheria peke yake. Kama wenzangu walivyosema, kuma mambo mengi ambayo yanafaa kuelezewa kwa lugha ya Kiswahili. Jambo lingine ambalo tunataka kuangalia ni wakati ambapo tunafanya mitihani. Mitihani yetu iko kwa lugha za Kiingereza na Kiswahili. Ningeomba kamati inayohusika na elimu itilie mkazo ili Kiswahili kiwe lugha rasmi. Walimu pia wanalegea katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili. Utapata kuwa watoto hawapendi kuifanya lugha ya Kiswahili na wanaongea “SHENG”. Ningeomba Kiswahili kitiliwe mkazo zaidi hata katika vyuo vikuu. Hata sisi hapa Bungeni, hatuongei Kiswahili siku zote. Tunaongea kwa lugha ya Kiingereza. Tutawezaje kuzielewa zile sheria kama tutaendelea kuongea Kiingereza? Hata wafanyikazi tunaoletewa kutusaidia hapa Bungeni, wanapaswa kuijue lugha ya Kiswahili ili wanapotafsiri, watafsiri Kiswahili ambacho tutakielewa sisi kama Wabunge. Jambo lingine ambalo ningetilia mkazo nikimaliza ni jambo la Bajeti. Tunapoitengeza Bajeti yetu, ni vizuri wenzetu wafahamu kuwa tunaweza kuitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Tusiwe tunangoja kuelezewa katika lugha ya Kiingereza. Tunafaa kuilewa Bajeti kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa lugha ya Kiswahili. Ninaunga mkono Hoja hii. Pia, ninamshukuru mwenzangu, Mhe. Joyce Lay. Amefanya jambo la maana sana kuileta Hoja hii ili tuijadili leo."
}