GET /api/v0.1/hansard/entries/530887/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530887,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530887/?format=api",
    "text_counter": 174,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Shukrani sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza naomba kumpongeza Mheshimiwa Joyce, kwa sababu ya hii Hoja aliyoileta. Kusema ukweli, shida tuliyonayo Kenya ni kuwa sheria tukonazo nyingi lakini utekelezaji ndio shida. Ikiwa tuliweza kukipitisha Kiswahili kiwe lugha ya Taifa tangu enzi za Raisi aliyestaafu Mheshimiwa Moi na mpaka leo hakijatiliwa maanani, tungependa tujiulize: Shida iko wapi? Pia tuangalie jinsi ambavyo tunaweza kuirekebisha shida hiyo ili Kiswahili kiweze kutumika hata kwenye chupa za dawa. Maelezo yawe yameandikwa kwa Kiswahili ndio yule mama kijijini asiweze kumpatia mtoto wake dawa kipimo cha zaidi. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu mengi tunayoyazungumza hapa Bungeni ni yanayomhusu mwananchi kule nyanjani. Lakini je, ni wote wanaoelewa kile ambacho tunakizungumza kwa Kizungu? Hata wakati tunapokwenda kutafuta kura zetu, sidhani kwamba tunazitafuta kwa kuzungumza Kiingereza. Tunaomba kura zetu hususan kwa kutumia lugha yetu ya taifa. Kwa hivyo, hii Hoja itaweza kutusaidia sio sisi tu kama Wabunge kuweza kueleweka kule nyanjani, bali pia wananchi ambao wanajua kukizungumza na kukisoma Kiswahili lakini hawawezi kukitafsiri Kiingereza kwa lugha ya Kiswahili. Ukiangalia katika korti zetu, utakuta mtu amehukumiwa na hajui amehukumiwa kivipi. Hata namna ya kuweza kuibadili ile hukumu anashindwa. Inaishia mtu huyo kutozwa pesa nyingi sana na mawakili bila kujielewa kwa sababu ataelezwa mambo ambayo si ya kweli. Lakini kwa vile anatafuta haki yake, anakubali na mwisho inaishia kuwa atafungwa licha ya kwamba ametoa pesa nyingi kwa mawakili waliomwambia kwamba wakibadilisha sehemu fulani, watapata haki yake. Kwa hivyo, ninaunga mkono Hoja hii na nina imani na Waheshimiwa licha ya kwamba tutaweza kubadilisha mipangilio yetu ya Bunge iweze kuandikwa kwa Kiswahili, tuanzie hapo na tuweze kuona pia hata masomo katika shule zetu kama vile Jiografia na Agriculture zimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Hii ni ili tuweze kuelewa lugha hizi zote na tuweze kutumia haki zetu tukiwa tunaelewa haki zetu tunazitumia kwa njia gani. Ningependa nikomee hapo kwa sababu naona muda hauturuhusu kuzungumza sana na kila Mheshimiwa anataka kuchangia Hoja hii. Shukrani."
}