GET /api/v0.1/hansard/entries/530893/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530893,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530893/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "Asante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Umuhimu wa mawasiliano ni kuwasilisha ujumbe ama habari kwa lugha inayoeleweka. Huo ndio umuhimu wa mawasiliano. Ukitaka mtu alielewe jambo, lazima utumie lugha anayoielewa. Kama tunataka Wakenya wajue sheria zetu, ni lazima tutumie lugha ambayo wanaielewa. Ingawa tunaongea mambo ya kutafsiri sheria zetu katika lugha ya Kiswahili, kuna changamoto ambazo ni lazima kwanza tukabiliane nazo ndipo lugha hii iwe ya maana kwa wananchi. Chanagamoto ya kwanza ni kuwa zaidi ya asilimia sabini ya Wakenya hawajui kusoma. Kwa hivyo, hata ukitafsiri sheria zetu kwa lugha ya Kiswahili bado kuna shida. Jambo kuu ni kuanza kuhamasisha watu wetu waende shule. Watu wazima ambao wamepita umri wa kusoma waanze kuhudhuria madarasa ya watu wazima! Wakisha jua kusoma, hizo sheria zilizotafsiriwa katika lugha ya Kiswahili zitakuwa za umuhimu kwao. Kama huyu hajui kusoma, hata ukitafsiri sheria hizo kwa Kiswahili, bado haina ladha wala faida kwake. Changamoto nyingine ni kwamba maktaba ya taifa hayahifadhi Katiba katika lugha za makabila yetu. Itafika wakati ambapo watoto watakaozaliwa hawatajua lugha The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}