GET /api/v0.1/hansard/entries/530894/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530894,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530894/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "zao. Ni muhimu maktaba ya kitaifa ijaribu njia zote za kuhifadhi kila chombo chenye thamani. Kwa mfano, kuihifadhi Katiba katika kila lugha nchini itawasaidia wale ambao watazaliwa, baada ya sisi kuondoka, kufahamu jinsi lugha zao zilivyokuwa. Watoto wengine wanaozaliwa mijini, kama Nairobi, hawajui lugha zao. Wanajua Kiswahili na Kiingereza pekee. Inakuwa shida kuhifadhi utamaduni na lugha zetu. Tukiendelea namna hii, lugha zingine zitakuja kupotea. Siwezi kuzungumzia lugha nyingine, lakini lugha yangu ya Kiturkana itaendelea kuweko. Changamoto nyingine ni kwamba Kiswahili simulizi ni tofauti na Kiswahili cha kuadika. Kwa mfano, Kiswahili kinachotumika katika eneo la Pwani si Kiswahili ambacho kinaweza kutumika kutafsiri sheria zetu. Kiswahili cha Pwani ni lugha simulizi. Katika lugha ya Kiswahili, kuna ngeli na herufi. Kwa hivyo, wakati tunaposema tukalimani na kutafsiri sheria zetu, ni lazima tuwe na walimu ambao wanaelewa ngeli, na wanajua kuisanifisha lugha ya Kiswahili ili mtoto atakayesoma Kiswahili aweze kutofautisha Kiswahili cha kuongea na Kiswahili cha kuandika. Kwa hivyo, kuna changamoto pia ya kuhakikisha kwamba tunafundisha Kiswahili katika shule zetu ili watoto wetu waweze kujua Kiswahili sanifu na kupata nafasi ya kuajiriwa kama wakalimani ili waweze kutafsiri sheria zetu kwa lugha tofauti. Changamoto nyingine ni kwamba walimu wa Kiswahili katika nchi hii ni wachache. Kwa hivyo, hata tukikubaliana kutafsiri sheria zetu kwa lugha ya Kiswahili, tusipokuwa na walimu wakutosha ambao wataifundisha lugha hiyo kote nchini, hatutaweza kufaulu. Kwa hivyo, tuihimize Serikali iwaajiri walimu wengi wa lugha ya Kiswahili, ili wafundishe lugha hiyo shuleni zetu, ili watoto wetu wajue kusoma Kiswahili ndiyo tuwatumie watoto hao kutafsiri sheria na vitabu vyetu kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hayo machache, ningependa kuiunga mkono Hoja hii."
}