GET /api/v0.1/hansard/entries/530903/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530903,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530903/?format=api",
    "text_counter": 190,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, nikimkumbuka Rais wa Tanzania, mhe. Julius Kabarage Nyerere, ambaye alikitafsiri kitabu chake cha Uhuru WaWatumwa, natumaini kwamba tunaelekea kupata uhuru wetu. Sheria za nchi yetu zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Hoja hii inaomba wanaohusika watafsiri sheria zetu zote, pamoja na Katiba, kwa lugha ya Kiswahili; ambayo ndiyo lugha inayoeleweka na wengi. Tukiangalia ule udhalimu waliofanyiwa Wakenya, utaona kwamba mara nyingi waadhiriwa wanashindwa kueleza kwa lugha ya Kiingereza kwa sababu lugha ambayo wanaifahamu ni Kiswahili. Mara nyingi, washukiwa wanapopelekwa mahakamani, wakalimani ambao wameajiriwa kutafsiri lugha ya Kiingereza mara nyingi huwapotosha washtakiwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}