GET /api/v0.1/hansard/entries/530904/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530904,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530904/?format=api",
"text_counter": 191,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mhe. Spika, tulipoipitisha Katiba mwaka wa 2010, tukaingia katika sera ya ugatuzi, moja ya vipengele ambavyo vinahusika ni makadirio ya fedha za kaunti. Makadirio hayo huandikwa kwa lugha ya Kiingereza, na watu hawaelewi. Utakuta fedha ambazo zinaombwa na kaunti zimeandikwa kwa Kiingereza na wananchi wanashindwa watajikwamua namna gani kutoka kwa hali hiyo ili wapate kuyaelewa makadirio hayo. Wakitaka kuyapitisha, mara nyingi wanayapitisha kwa sababu ya maelezo wanayopata kutoka kwa wahusika, ambao huwadanganya wananchi kua wamefanya marekebisho kwa sababu ya shida ya lugha. Mazungumzo yetu ya kawaida hufanywa kwa Kiswahili. Ninapochangia Hoja na Miswada hapa Bungeni, mara nyingi mimi hutumia lugha ya Kiswahili. Namshukuru mhe. Lay kwa kuileta Hoja hii Bungeni, kuwashinikiza wanaohusika kuzitafsiri sheria zetu kwa lugha ya Kiswahili. Tukubaliane kwamba vituo vingi vya redio vinavyotumia masafa marefu, ambavyo hupeperusha vipindi vyao kwa lugha ya Kiswahili, vina wafuasi wengi ambao wanavifurahia kuliko vituo ambavyo hupeperusha vipindi vyao kwa Kiingereza. Wakati umefika wa kuchapisha matangazo ya kandarasi za Serikali magazetini kwa lugha ya Kiswahili ndiyo wananchi wapate kujua ni nini kinahitajika kutoka kwao. Nikimalizia, hata Bibilia na Kuruani zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Itakuaje Katiba yetu, ambayo imebana humu nchini, ibaki kwa kugha ya kigeni pekee? Ndiyo maana Hoja hii ni muhimu sana. Ninawaomba Wabunge wenzangu waiunge mkono Hoja hii na watilie mkazo ili kila kitu chetu kipate kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Kwa haya machache, ninaaunga mkono."
}