GET /api/v0.1/hansard/entries/530906/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530906,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530906/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Ahsante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuunga mkono, na haswa pia kulizungumzia suala hili ambalo dada yangu mhe. Lay ameweza kulileta hapa Bungeni – kuhusu umuhimu wa kuzitafsiri sheria zetu kwa lugha ya taifa. Ninampongeza Bi. Lay kwa kuileta Hoja hii ambayo ni ya muhimu sana. Ukiangalia Kipengele cha 7(2) ambacho kinazungumzia masuala ya jamuhuri yetu ya Kenya, ni wazi kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa. Kipengele cha 7(2) kinabainisha kwamba lugha rasmi za taifa letu ni mbili; Kiswahili na Kiingereza. Utaona kwamba Kiswahili kimetangulia Kiingereza kwenye mpangilio huo. Hii inamaanisha kwamba Kiswahili kina umuhimu mkubwa nchini Kenya. Kipengele cha (7) hakikuwekwa kwenye Katiba yetu kuwa pambo bali kimewekwa kwenye Katiba kuonyesha wazi umuhimu wa Kiswahili kwa nchi yetu. Kwa hivyo, kama alivyopendekeza Bi. Lay, Kiswahili kitumike rasmi kwenye sheria zetu zote. Ninapendekeza Serikali ilazimishwe kutekeleza suala hili. Suala hili halikuwekwa kwenye Kipengee cha 7 bure. Kuna umuhimu wa kuzitafsiri sheria zote za Kenya kwa lugha ya Kiswahili."
}