GET /api/v0.1/hansard/entries/530908/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530908,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530908/?format=api",
"text_counter": 195,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Mara nyingi, watu wengi huwa na uoga wa kuzungumza lugha hii ya Kiswahili wakifikiria kuwa kuna yule ambaye labda ana ujuzi kushinda mwingine. Nafikiria lugha huwa inazidi kukuzwa kama watu wataitumia. Ukienda Rwanda, utakuta kuwa Kiswahili kinatumika kila mahali kwa sababu pia wao wameamua kuwa Kiswahili ni lugha yao ya taifa. Kama Rwanda ambayo ni nchi ilikuwa na matatizo inatumia lugha hii, sembuse sisi Wakenya ambao tulianzisha suala hili kitambo?"
}