GET /api/v0.1/hansard/entries/530916/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530916,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530916/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kemei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2778,
        "legal_name": "Justice Kipsang Kemei",
        "slug": "justice-kipsang-kemei"
    },
    "content": "Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia Hoja hii. Kwanza, ningependa kumshukuru mhe. Lay kwa kuleta Hoja hii Bungeni na kuitanguliza.Vile vile, ningependa kumshukuru mhe. Mbadi kwa kuifanyia marekebisho kusudi sisi tunapoichangia iambatane na mahitaji yetu kama taifa. Ingawa tumeitambua lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa na vile vile kama lugha yetu katika Afrika ya Mashariki, katika matumizi yake hatujaboresha lugha hii iwe kama lugha ya Kiingereza. Masikitiko yangu ni kwamba, hata mwenye kuileta Hoja hii Bungeni na mwenye kuifanyia marekebisho, wote wawili walitumia lugha ya Kimombo. Ningefurahi sana kama wangeitumia lugha ya Kiswahili kusudi sisi sote tuendeshe mambo yetu katika lugha ya Kiswahili ili kuimarisha lugha hiyo. Nitaongea kwa ufupi kwa sababu kuna wenzangu ambao vile vile nao wangependa kuchangia Hoja hii. Jambo langu kuu ni kwamba Kenya na dunia nzima inapiga hatua sana katika nyanja ya sayansi, teknolojia na mawasiliano. Maendeleo hayo hayatakuwa na manufaa kwetu na kwa watu wetu ikiwa hatutatumia lugha ambayo watu wetu wanaelewa. Vile vile ningependa kituo hiki cha kunakili na kupasha habari kuhusu sheria zetu kipewe nguvu ili kufanya kazi kana kwamba mawasiliano yote ya umma, sio sheria peke yake, yaweze kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kusudi watu wetu waweze kuelewa mambo ambayo yanaendelea katika nchi yetu. Naunga mkono Hoja hii. Namsihi mhe. Lay vile vile alete mswada Bungeni kusudi tutengeneze sheria. Ahsante. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}