GET /api/v0.1/hansard/entries/530929/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530929,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530929/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Kunao umuhimu wa kuhakikisha kwamba lugha ya Kisawahili imetumiwa vyema na hasa kutafsiri Katiba yetu na sheria zetu ili kuhakikisha kwamba watu wengi wanaelewa mambo haya. Ukiangalia ndani ya Katiba yetu, kuna baadhi ya vipengele ambavyo vimesisitizwa kwamba iwapo kuna changamoto ya lugha, ni muhimu pia Serikali ihakikishe kwamba imepeana watu ambao wanaweza kutafsiri ama wakalimani hasa mahakamani."
}