GET /api/v0.1/hansard/entries/530931/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530931,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530931/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chea",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1694,
        "legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
        "slug": "mwinga-gunga-chea"
    },
    "content": "Kwanza, mawasiliano yatakua mema kati ya wale wote ambao wanahusika katika utumizi wa maswala ya kisheria. Mengi yamezungumzwa hapa kuhusu vile mawakili na baadhi ya watu hutumia lugha hii ya Kiswahili kujiletea utajiri. Nikionekana labda natetea mawakili hawa, kati ya matawi yote ya kiserikali yakiwemo hasa mahakama, na ambayo hasa mara nyingi utata wa lugha hii hutokea, kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba mahakimu wetu mara kwa mara, wanapelekwa katika warsha ndio waelewe vile maswala kama haya yanaendelea. Kwa hiyo, ningependa kusisitiza kwamba kuna haja ya kuhakikisha kuwa hata askari wetu ambao mara nyingi ndio huwa vianzilishi vya kesi hizi, wanafahamu lugha hii. Wakati wanapoandika malalamishi ya washukiwa, waiandike kwa lugha ya Kiswahili."
}