GET /api/v0.1/hansard/entries/530945/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530945,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530945/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwamkale",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2672,
"legal_name": "William Kamoti Mwamkale",
"slug": "william-kamoti-mwamkale"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii. Kwanza, ninampongeza Mhe. Lay kwa kuleta Hoja hii ambayo wakati wake umefika. Imesemwa hapa kwamba Kifungo cha Saba cha Katiba yetu kii wazi ya kwamba lugha ya Kiswahili sio lugha ya kitaifa tu, bali ni lugha rasmi ya nchi hii. Kifungu hicho kinaendelea kusema kwamba Serikali ina jukumu la kuhakikisha kwamba Kifungu hiki kinatekelezwa. Hivyo basi, ninapendekeza ya kwamba, hata baada ya hoja hii kupita, Bunge hili lije na sheria ya kuisurutisha Serikali itekeleze haya yote."
}