GET /api/v0.1/hansard/entries/530950/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530950,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530950/?format=api",
"text_counter": 237,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwamkale",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2672,
"legal_name": "William Kamoti Mwamkale",
"slug": "william-kamoti-mwamkale"
},
"content": "tuhakikishe kwamba sheria hizi ziko katika lugha inayojulikana na wengi. Natambua ya kwamba kati ya lugha zote, lugha ya Kiswahili inajulikana na wengi, sio katika eneo la Pwani peke yake bali mpaka Nyanza na Mandera. Wengi wanaelewa lugha hii. Hata wale ambao hawakupata elimu ya kawaida wameenda ngumbaru na wanazungumza Kiswahili. Kama vitabu vyetu vya sheria na sheria tunazozitunga hapa zitakuwa katika lugha ya Kiswahili, nina imani kwamba Wakenya wengi watafuata sheria na megereza yetu hayatakuwa na watu ambao hawana hatia lakini wako huko kwa sababu ya ukosefu wa kuelewa sheria ambayo wanatakikana waifuate."
}