GET /api/v0.1/hansard/entries/530952/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530952,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530952/?format=api",
"text_counter": 239,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. ole Ntutu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2535,
"legal_name": "Patrick Keturet Ole Ntutu",
"slug": "patrick-keturet-ole-ntutu"
},
"content": "Asante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii uliyonipa. Nampogeza mhe. (Bi.) Lay kwa kuleta mjadala huu. Mjadala huu ni muhimu sana kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi wa Kenya hawajasoma na hawaelewi lugha ya Kiingereza. Kama tulivyosikia kutoka kwa mhe. (Bi.) Lay, wale ambao wanastahili kutafsiri Katiba na sheria nyingine hawana fedha. Ni jukumu letu kama Wabunge kuhakikisha kwamba wana fedha ili waweze kufanya kazi hii. Juzi nilikuwa nikifuatilia mjadala wa Bunge la nchi jirani ya Tanzania. Kwa kweli, nilifurahishwa sana na jinsi Wabunge walivyokuwa wakiendesha mjadala wao. Mjadala ambao ulikuwa unaendelea ulikuwa muhimu sana kwa sababu Wabunge walikuwa wanachangia wakijua wanachozungumzia. Najua wenzangu wengi hapa hawapendi kuzungumza kwa lugha yetu ya taifa. Wakati umefika kwa sisi pia hapa Bungeni kujifunza kuzungumza kwa lugha yetu ya Kiswahili. Ukienda katika nchi za ng’ambo, kama Uholanzi, utaona kwamba ijapokuwa Kiingereza kinatumiwa, wanahakikisha kwamba wanatumia lugha ambayo inajulikana na watu wengi. Ukiangalia shuleni, kortini au hata katika kuandika kandarasi, utaona kwamba lugha inayotumiwa ni ile ambayo wengi hawaijui. Ndiposa nataka niseme kwamba---"
}