GET /api/v0.1/hansard/entries/530957/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530957,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530957/?format=api",
    "text_counter": 244,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Nyasuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 590,
        "legal_name": "Gladys Atieno Nyasuna",
        "slug": "gladys-atieno-nyasuna"
    },
    "content": "Asante sana mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii. Moyo wangu ulikuwa unadundadunda kwa sababu nilikuwa nimetafuta Kiswahili chote na nilikuwa naona muda unaisha kabla sijatumia Kiswahili hicho. Ninatoa shukrani kwa mhe. (Bi.) Lay kwa kuileta Hoja hii ambayo inatupatia nafasi ya kuzungumza kwa Kiswahili. Wabunge ambao wanatuongoza katika lugha hii ni mhe. (Bi.) Khamisi na mhe (Dkt) Shaban lakini leo mhe (Bi.) Lay ametuweka katika nafasi ya sisi pia kutumia Kiswahili. Nataka iende katika kumbukumbu za Bunge hili kwamba mimi nilipata alama ‘A’ katika somo la Kiswahili katika mtihani wa kidato cha nne (KCSE). Kiswahili cha kuandika nakijua lakini kile cha kuongea ni tofauti. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ukiwa kwa kiti leo, tunakupatia changamoto hata wewe pia uongee kwa Kiswahili ukituongoza katika mjadala huu kwa sababu kama mimi naongea, sembuse mhe. Naibu Spika wa Muda! Mjadala huu ni wa kikatiba. Ukiangalia Kipengele cha (35), utaona kwamba kila mwananchi ana haki ya kupata habari kutoka kwa ofisi ya umma na habari zozote ambazo mtu mwingine anazo ambazo zinahitajika ili kutekeleza au kulinda haki yoyote au uhuru wowote wa kimsingi. Katiba inasema kwamba kila mtu ana haki ya kupata habari. Habari hiyo ikiletwa kwako katika lugha ambayo huielewi, basi hujapata habari hiyo na hivyo basi Katiba itakuwa imekeukwa. Kile ambacho kinatatanisha ni huu mtazamo kwamba Kiswahili ni lugha ya watu wenye tabaka ya chini ilhali Kiingereza ni lugha ya watu wenye tabaka ya juu. Hapa Nairobi, utaona watu wa Eastlands wakizungumza kwa Kiswahili na watu wa Kileleshwa, Lavington na Runda wakizungumza kwa Kiingereza. Ule mtazamo wa kukiweka Kiswahili kama lugha ya watu wenye tabaka ya chini si mzuri kwa sababu hii ni lugha ya kitaifa. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ukiingia ndege ya Kenya Airways huko Uchina halafu usikie wanasema “karibu sana katika ndege hii yetu ya Kenya Airways”, unasikia uko na fahari."
}