GET /api/v0.1/hansard/entries/530967/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530967,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530967/?format=api",
"text_counter": 254,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Theuri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1429,
"legal_name": "George Theuri",
"slug": "george-theuri"
},
"content": "Kiswahili ni lugha ya taifa na ni muhimu tuelewe kwamba sio Wakenya wote wanaofahamu Kizungu. Kusudi sote tuweze kuwa na usawa, ni muhimu sheria ya nchi ichapishwe kwa lugha ya taifa. Tuna watu wengi ambao wangependa kujua na kujisomea sheria. Ili tuwezeshe hawa Wakenya wenzetu kufaidika, ni lazima tuchapishe sheria kwa lugha iwezayo kueleweka kwa urahisi ambayo ni lugha ya taifa. Ili tuweze kujivunia uhuru wetu, ni muhimu tuchapishe sheria kwa lugha ya Kiswahili tunayojivunia. Ni lazima tujikomboe na tuchapishe sheria kwa lugha ya taifa. Naunga Hoja hii mkono. Asante sana."
}