GET /api/v0.1/hansard/entries/530979/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530979,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530979/?format=api",
"text_counter": 266,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. M’uthari",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1576,
"legal_name": "Joseph M'eruaki M'uthari",
"slug": "joseph-meruaki-muthari"
},
"content": "Okay. Asante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Mimi pia nimesimama kuunga mkono Hoja hii. Hii Hoja ni muhimu sana kwa sababu tunajua lugha ya Kiswahili ni lugha ya kitaifa na inayoeleweka sana katika nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, tukitafsiri Katiba yetu iwe kwa lugha ya Kiswahili, itakuwa ya manufaa kwa sababu watu wengi Kenya wataweza kuelewa. Pia tunajua umuhimu wa lugha. Lugha ndiyo njia ya kueneza utamaduni wa watu. Nchi nyingi kama Uchina na Ulaya wanatumia lugha zao. Pia tunasambaza utamaduni wa Waingereza kwa kutumia lugha yao. Ukiona Waitaliano na Wafaransa, wao pia wanatumia lugha zao. Kwa sababu Kiswahili kimekuwa sio lugha ya Kenya pekee bali lugha inayotumika eneo la Afrika naamini kuwa hata nchi nyingi za Afrika kama eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki utaona kuwa nchi nyingi zinatumia lugha ya Kiswahili. Tunaangalia hata zile nchi za Afrika ya Kati wanapotumia Kiswahili. Tunahitaji tuwe hata na pesa iliyowekwa kueneza lugha ya Kiswahili tutakapokitumia kwa Katiba kwa sababu njia hiyo itasaidia kukuza utamaduni wetu na sisi watu wa Kenya. Ukiangalia utaona kuwa watu wengi Kenya hawaelewi hata majukumu tofauti yaliyopeanwa na hii Katiba yetu ya 2010. Ukiangalia kazi za zile serikali za mashinani na Serikali Kuu utaona kuwa watu hawaelewi."
}