GET /api/v0.1/hansard/entries/530981/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530981,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530981/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii iliyoletwa ni dadangu Mheshimiwa Joyce Lay. Kwanza nataka kusema ikiwa Kiswahili ni lugha rasmi na ya kitaifa ni lazima tuitukuze na kuienzi kwa mahaba kama tunavyoipenda lugha ya Kiingereza ambayo tuliletewa na wakoloni. Nataka kusema kuwa Katiba yetu ya sasa ni sheria mama na ndiyo inasimamia utawala wa nchi yetu. Vipi Katiba hii itakuwa haijatafsiriwa kwa Kiswahili? Hili ni suala ambalo lazima sisi watungasheria katika Bunge hili tunafaa tuliangalie kwa undani sana. Katika utekelezaji wa sheria, lazima washikadau husika wahusishwe katika mambo ya sheria."
}