GET /api/v0.1/hansard/entries/530984/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 530984,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530984/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, katika barabara zetu hapa Kenya tunaona kwamba kuna sheria ambazo zimewekwa. Kwenye kibao, utaona kumeandikwa “Keep Left” kwa Kiingereza ama “Keep Right”. Kwa Mkenya ambaye hajui lugha ya Kiingereza, huoni kwamba anaweza kufanya ajali kwa sababu ya kutoijua lugha iliyotumiwa kwenye alama ile? Akina mama wengi na mabanti wetu wadogo, ambao wanabakwa, wanaelewa Kiswahili. Wanapokwenda kwenye afisi za wahusika wa kisheria kuandikisha taarifa kuhusu dhuluma ambayo wamefanyiwa, wengi wao hawawezi kuandikisha taarifa kwa Kiingereza. Hivyo basi, mhasiriwa anapoandikisha taarifa yake kwa Kiswahili, afisa wa polisi anamwambia: “Dada, ninaweza kukutafsiria taarifa hii kwa lugha ya Kiingereza.” Je, banati huyu, ambaye ni mchanga wa umri, na ambaye hafahamu sheria zetu, atawezaje kujua kwamba taarifa yake imeandikwa kwa lugha inayofaa na kwa yale malengo yanayohusu dhulma aliyofanyiwa? Hata katika jela zetu---"
}