GET /api/v0.1/hansard/entries/530995/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 530995,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/530995/?format=api",
    "text_counter": 282,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ramadhani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2388,
        "legal_name": "Suleiman Dori Ramadhani",
        "slug": "suleiman-dori-ramadhani"
    },
    "content": "Ahsante, mhe. Naibu Spika wa Muda. Kiswahili ni lugha ambayo ina umuhimu kwetu sisi Wakenya. Ni lugha ambayo inatuelekeza katika shughuli zetu za kila siku. Kwa hakika, idadi kubwa ya Wakenya hutumia Kiswahili katika kila jambo wanalolifanya kwa sababu hiyo ndiyo lugha ambayo inafahamika vyema. Kwa hivyo, tunapotunga sheria na kufanya jambo lolote, ni lazima tufahamu kwamba wakenya ndio muhimu. Tunafaa kuhakikisha kwamba jambo hili limefahamika."
}