GET /api/v0.1/hansard/entries/531008/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 531008,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/531008/?format=api",
    "text_counter": 295,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. (Ms.) T.G. Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 460,
        "legal_name": "Tiyah Galgalo Ali",
        "slug": "tiyah-galgalo-ali"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuichangia Hoja hii. Ningependa kumshukuru dada yangu Mhe. Lay kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Ni haki ya Wakenya kupata Katiba iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Hili si ombi wala ni lazima. Ningependa kuwakosoa walioandika Katiba ya Kenya na kukosa kuiandika kwa lugha ya Kiswahili. Hii ni haki ya Wakenya wote. Watu wasipoelewa Katiba, ni vigumu sana kwao kujitetea popote Kenya. Hoja hii ni muhimu. Ningependa kuwahimiza wale ambao wanahusika, wahakikishe kwamba Katiba ya Kenya ambayo ni sheria kuu ya kuwasaidia wananchi wote wa Kenya, imetafsiriwa kwa Kiswahili ndio Wakenya waelewe vizuri jinsi ya kujitetea. Kwa hivyo, Hoja hii imeletwa wakati unaofaa. Ingeletwa hapo mbeleni lakini ningeomba tuipitishe ndio tuhakikishe kwamba Wakenya wanafaidika."
}