GET /api/v0.1/hansard/entries/531010/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 531010,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/531010/?format=api",
    "text_counter": 297,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. (Ms.) Katana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 691,
        "legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
        "slug": "aisha-jumwa-katana"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka kuichukua nafasi hii kwanza nimpongeze Mhe. Lay kwa kuileta Hoja ambayo ni muhimu sana katika taifa letu la Kenya na katika Bunge hili kwa jumla. Wakenya waliandika historia tarehe 27/8/2010 kwa kupitisha Katiba ambayo ni mwongozo katika taifa hili letu la Kenya. Lakini, Wakenya wengi kuhakikisha kwamba Katiba inawalinda, lazima waifahamu. Lugha ambayo inafahamika kwa urahisi na wananchi wengi katika taifa hili ni lugha ya Kiswahili. Hakuna mtu ambaye anaweza kujivunia Kiswahili na kusema ni lugha yake. Ni lugha ambayo imetumika katika taifa hili na 1974, ilitangazwa rasmi kuwa lugha ya kifaifa. Inatumiwa na makabila mbalimbali katika taifa hili. Kiswahili kinaleta jamii za Wakenya pamoja. Hivyo basi, ni vyema sheria na stakabadhi zote muhimu katika taifa hili zitafsiriwa katika lugha inayoeleweka na wengi. Katika ununuzi wa zabuni, ambao hata Rais wetu wa Jamhuri ya Kenya amesisitiza sana kwamba asilimia 30 zienda kwa kina mama na vijana, ukiangalia sheria za ununuzi wa zabuni katika taifa hili, zimeandikwa kwa lugha ambayo kina mama na vijana katika Jamhuri yetu ya Kenya hawazielewi. Hivyo basi, wale mabwenyenye waliobobea katika fani hizo na wenye kuelewa lugha ya kimombo wanajivunia na kufaidi katika taifa hili na kuwacha wengine wakiwa katika hali za upweke."
}