GET /api/v0.1/hansard/entries/531015/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 531015,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/531015/?format=api",
"text_counter": 302,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bedzimba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1933,
"legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
"slug": "rashid-juma-bedzimba"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nashukuru kupata fursa hii. Waswahili wanasema “chelewa ufike”. Nimefika sasa. Lugha ya Kiswahili si lugha tu ya taifa, ni lugha rasmi ya taifa la Kenya. Kiswahili kimeangaziwa sana kama ni lugha ya watu maskini ingawa si kweli bali ni unyanyasaji kwa wale wanaotumia Kiswahili. Kutafsiri sheria za Kenya kwa lugha ya Kiswahili kutawawezesha wengi kuelewa ikiwa waliosoma na hata ambao hawakusoma. Ile lugha inayotumika ya Kiingereza ni ya ndani sana ambayo si rahisi mtu kuielewa. Kwa hivyo, ni vyema sana sheria hii itafsiriwe kwa Kiswahili. Viongozi wote ambao wako hapa, karibu asilimia 90, wameletwa hapa kwa sababu ya lugha ya Kiswahili. Si rahisi kuwapata viongozi ambao wanatoa ahadi wakati wanaomba kura kwa lugha ya Kiingereza. Wengi wanazungumza Kiswahili lakini wanapokuja hapa kidogo wanaona kwamba lugha ya Kiswahili ni ya chini. Hii si kweli. Mataifa mengi ambayo yanatumia lugha zao yameendelea mbele sana. Ukiangalia Bara la Waarabu, Uchina na Hispania, wanatumia lugha zao ndio sababu wameendelea mbele haraka. Hata nchi jirani ya Tanzania, uchumi wake unakua kwa kasi sana kwa sababu ya kutumia lugha yao. Sisi tunatumia lugha ya wakoloni waliotufunga. Tumeikuza lugha yao na yetu tukaipuuza. Ndio sababu hawachukui nafasi kujifundisha lugha zetu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}