GET /api/v0.1/hansard/entries/531018/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 531018,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/531018/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mustafa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1864,
"legal_name": "Salim Idd Mustafa",
"slug": "salim-idd-mustafa"
},
"content": "Ahsante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja hii muhimu. Ningependa kuchukuwa fursa hii kumshukuru mheshimiwa Joyce Lay kwa kuileta Hoja hii katika Bunge. Kiswahili kinapendeza na kinafaa kutukuzwa ndipo kitumike katika nyanja muhimu kama vile sheria. Mimi nitakupa ninayoyajua katika sheria kuhusiana na Kiswahili. Niliwahi baada ya kushinda uchaguzi kupelekwa mahakamani na wapinzani wangu. Lugha iliyokuwa ikitumiwa ni Kiingereza. Wengi wa wafuasi wa wapinzani wangu walipofika mahakamani hawakuelewa kesi. Hii ni kwa sababu kila siku tulipokuwa tunatoka mahakamani wao wangerudi mitaani na kueneza mambo ambayo hayakuwa mahakamani kwa sababu walikuwa hawaelewi lugha ya Kiingereza. Kwa sababu hiyo naona umuhimu wa kutafsiri sheria zetu katika lugha ya Kiswahili."
}