GET /api/v0.1/hansard/entries/531019/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 531019,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/531019/?format=api",
"text_counter": 306,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mustafa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1864,
"legal_name": "Salim Idd Mustafa",
"slug": "salim-idd-mustafa"
},
"content": "Mimi naonelea kwamba ni muhimu tutenge angalau kikao kimoja kutoka katika vikao vinne ambavyo Bunge inavyo kila wiki ili kikao hicho kimoja kiendelezwe kwa lugha ya Kiswahili. Tukifanya hivyo basi tutasaidia kukuza Kiswahili. Aidha, kitendo hicho kitawashurutisha Wabunge kukienzi Kiswahili. Baadhi ya shule humu nchini zimetenga siku kadhaa kuwa siku za wanafunzi kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu wanafunzi hutahiniwa kwa lugha zote mbili; Kiingereza na Kiswahili. Ingekuwa vizuri pia sisi tuonyeshe mfano bora kama ilivyo katika mabunge mengine katika eneo la Afrika Mashariki na Kati."
}