GET /api/v0.1/hansard/entries/531023/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 531023,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/531023/?format=api",
"text_counter": 310,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Odanga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2286,
"legal_name": "Geoffrey Makokha Odanga",
"slug": "geoffrey-makokha-odanga"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nami pia nataka kuiunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa hapa na Mhe. Wanjala na kufanyiwa marekebisho na Mhe. John Mbadi. Naiunga mkono kwa sababu Kiswahili ni lugha yetu. Ni lugha ya Kiafrika na pia imetambuliwa katika Katiba kuwa lugha rasmi ya taifa. Ikiwa lugha rasmi, sioni urasmi wake sana isipokuwa katika Katiba. Taasisi ya Mtaala katika Shule za Kenya imekitambua Kiswahili kuwa lugha ya lazima kwa wanafunzi katika shule za msingi na shule za upili. Hiyo inamaanisha kuwa Wakenya wengi sana wanakielewa Kiswahili. Inafaa kwamba stakabadhi zote rasmi zitafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili ikiwemo Katiba ya Kenya. Pia, Katiba inaelekeza kuwa Wakenya wote wana haki ya kupata habari. Ikiwa wana haki ya kupata habari, basi habari hiyo iwekwe katika lugha ambayo wanaelewa vizuri na wanaitumia katika maisha yao ya kila siku. Ikiwa hii ni lugha yetu, ni vizuri kuichangamkie zaidi kuliko lugha za kigeni kama vile Kiingereza ambayo ni lugha inayoendeleza ukoloni mambo leo. Ikiwa tunataka kujikomboa kutoka minyororo ya ukoloni, ni lazima tuienzi na kujivunia lugha yetu ya Kiswahili. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}