GET /api/v0.1/hansard/entries/531054/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 531054,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/531054/?format=api",
"text_counter": 26,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Mheshimiwa Bw. Spika, niruhusu niangaze mawazo yangu kwa kazi nzuri iliyotekelezwa na Mama wa Taifa. Sijui kwa nini aliuita huo mpango wake Beyond Zero Campaign, lakini hata hivyo, twamshukuru. Hizi kaunti 20 ambazo amezitaja ndizo kaunti zilizo na wingi wa vifo kwa sababu zingine; vifo vya watoto, vifo kwa sababu ya magonjwa ya zinaa kama vile UKIMWI na kadhalika. Kwa sababu gani akachagua sehemu hizi 20? Hili ni swali ambalo lazima lijibiwe na Serikali. Ukweli ni kwamba hizi ni sehemu ambazo zilipuuzwa tangu zamani. Hivyo basi, Mama wa Taifa aliona haya ndipo akaanzisha Beyond Zero Campaign. Namuomba afanye hima ili afikishe gari la matibabu kwenye Kaunti ya Migori, kwa sababu hatujaliona huko na twalingoja kwa hamu. Tunamsihi kwamba asiogope kwani Migori ni mahali pazuri na anakaribishwa kabisa; hakuna viatu tena huko. Bw. Spika, utu ni kipawa na huyu mama ana kipawa cha utu. Kama vile Sen. Mutahi Kagwe alivyosema, lazima pia tumshukuru mume wake kwa sababu kama angekuwa mjeuri, hangeweza kufanya mradi huu. Uwezo wa mama humtegemea pia mwanaume; hawawezi wakatekeleza lolote bila ya kupewa ruhusa na baraka za mwanamume. Kwa hivyo, twamshukuru Mheshimiwa Rais kwa hilo. Pia, twataka kumuona akiambatana na mke wake siku moja wakikimbia katika mbio hizo; sio tu kumtuma mke wake kukimbia kila wakati. Twamtaka pia yeye akimbie na siku hiyo, sisi sote tutajitokeza kwa wingi na kukimbia naye. Kwa kazi nzuri, ya Kaisari, mpe; twamshukuru huyu mama."
}