GET /api/v0.1/hansard/entries/532152/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 532152,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532152/?format=api",
    "text_counter": 208,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Aburi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2901,
        "legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
        "slug": "lawrence-mpuru-aburi"
    },
    "content": "Asante, Bwana Spika. Yangu ni machache sana. Ninaunga mkono Hotuba ya Rais aliyotoa Alhamisi. Ukiangalia Wabunge katika Bunge hili, wamehangaishwa wakiwa chini ya mkanda mmoja wa magavana. Pesa zote za nchi ya Kenya zinapitia katika Bunge hili. Pesa za Voi, Kisumu, Embu, Laikipia na Meru zinapitia katika Bunge hili. Waheshimiwa katika Bunge hili wanajua ni pesa ngapi zinaenda katika kaunti zao. Lakini zikifika kwa kaunti, zinachukuliwa na wakora wasioshiba kule. Wanakaa chini pamoja na mawaziri na wawakilishi wa kaunti ambao hatuwaelewi na kugawa pesa hizi na kusema kuwa zingine zinaenda Malaysia, China, Texas, India, Dubai na zingine zinatumiwa kununua ng’ombe dume wa kuwazalisha ng’ombe wetu."
}