GET /api/v0.1/hansard/entries/532154/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 532154,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532154/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Aburi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2901,
        "legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
        "slug": "lawrence-mpuru-aburi"
    },
    "content": "Tumeteswa ya kutosha. Ukiangalia kule mashinani, Mbunge ako Nairobi siku saba. Akirudi kule mashinani, anamkuta mwakilishi wa kaunti ako na mambo yake pale na anaendesha Range Rover. Wawakilishi wa kaunti wanahudumia eneo dogo sana. Hawa wawakilishi wa kaunti wanapewa pesa nyingi sana na magavana ndio wawapige waheshimiwa. Pesa tunazozipata katika Bunge hili hazitoshi kuzunguka eneo la Bunge lote. Tumetosheka kutawaliwa vibaya na wakoloni Waafrika; ngozi nyeusi. Hawa magavana; washenzi wasioshiba, wanafaa kuongezwa kokoto kwa tumbo ndio wasihisi njaa tena. Wakati umefika tuungane kama Wabunge katika Bunge hili. Ukiangalia katika Kaunti ya Meru, tunalilia kwa choo na hatusikii harufu. Gavana wa Meru Kaunti amekua kama mungu mdogo na hata Rais Uhuru hamfikii. Ukienda kwa kila wadi, ameweka zulia nyekunda. Miradi iliyoko katika Kaunti ya Meru inafanywa na CDF. Kwa mfano, ukiangalia kwa Mhe. Mithika Linturi, kazi ambayo inafanyika kule inafanywa na CDF. Ukiangalia kwa Aburi, kazi ambayo inafanyika kule inafanywa na pesa za CDF. Pesa ya Serikali ya Kaunti ya Meru haionekani. Hizi pesa zote zinazotoka kwa Serikali kuu zinatumwa kwa serikali za kaunti na zinawekwa kwa mifuko ya magavana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}