GET /api/v0.1/hansard/entries/532157/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 532157,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532157/?format=api",
    "text_counter": 213,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 128,
        "legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
        "slug": "richard-onyonka"
    },
    "content": "Asante sana, mhe. Spika. Ndugu yangu, mhe. Aburi ameongea mambo mazito. Kwa sababu ametumia lugha ya taifa, ingekuwa vizuri nami nimfuatilie kuongea kwa lugha hiyo. Jambo la kwanza ambalo ningependa kusema ni kwamba nakubaliana na Hotuba ambayo Rais Uhuru Kenyatta alitoa hivi majuzi alipohutubia Bunge hili. Ukiangalia kwa makini, shida zilizoko humu nchini zimeambatana na kuunganishwa na ufisadi. Nakubaliana naye kwa sababu ukiangalia sababu inayofanya idara ya polisi kutofanya kazi, utagundua kwamba polisi wanakula mulungula njiani. Ukienda katika shule ambazo zina shida ya mtihani, na ambako wanafunzi hawajapewa vyeti vyao, utagundua kwamba sababu ni mtu fulani alikuwa anangojea apewe pesa ndio atoe vyeti hivyo kwa sababu ni lazima ale mulungula. Rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba ni lazima uchumi wa Kenya uendelee kukua. Shida za uchumi wa Kenya haziwezi kutatuliwa bila ya kupambana na ufisadi. Sababu za msongamano wa magari jijini Nairobi ni kwamba wale ambao walikuwa na jukumu la kutengeneza barabara miaka 30 iliyopita walipora hela, na barabara hazikutengenezwa. Mhe. Spika, nikija kwangu binafsi, nina kesi kortini. Kesi hiyo inasema kwamba nimefuja Kshs132 milioni. Inasemekana kwamba pesa hizo zilitoka katika Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (CDF). Ninataka wale wanaohusika na kuchambua mambo ya ufisadi serikalini wanisikize kwa sababu kisheria siwezi kuongea yaliyo kortini. Nitaongea yale yaliyofanywa na Tume ya kupambana na ufisadi ambayo ilivunjwa. Jambo la kwanza wanalosema ni kwamba katika mwaka wa 2008, nilikuwa Bungeni miezi mitatu. Wanasema kwamba wakati huo nilichukua Kshs132 milioni nikaenda kununua sukari ambayo mimi nilitumia. Ningependa kusema kwamba wakati huo, pesa nilizopata katika akaunti ya CDF ya Kitutu Chache zilikuwa Kshs24 milioni tu. Huo ulikuwa mwaka wa kifedha wa 2008/2009. Wanaendelea kusema kwamba nilifuja pesa hizo kutoka Agosti, 2008 hadi 2009. Hela ambazo CDF yangu ilipata katika mwaka wa 2009/2010 ni Kshs54 milioni. Ukijumlisha hazifiki Kshs.132 milioni. Jambo la pili ambalo ningependa kuzungumzia ni kwamba wale wanaotuchunguza katika ufisadi ni lazima wafuate sheria na wahakikishe kwamba kuna ukweli. Pia, ni lazima wajue kwamba mimi simhalifu hadi korti itakaponipata na hatia. Ni lazima wahakikishe kwamba wamepata ukweli wa mambo. Nawaomba wale ambao wana Ripoti iliyoletwa hapa Bungeni leo waangalie ukurasa wa tatu. Inasema kuwa nilifuja fedha za eneo Bunge la Kitutu Chache, ambazo zilikuwa Kshs132 milioni. Hiyo ndiyo sababu walinipeleka kortini. Ukienda katika ukurasa wa 43 wa Ripoti hii, wanasema----"
}