GET /api/v0.1/hansard/entries/532229/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532229,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532229/?format=api",
"text_counter": 285,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwashetani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": "Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda . Kwa sasa hivi, tukiangalia watoto wetu kwenye mashule, wamepata umeme na wanaweza kusoma usiku. Baadhi ya hayo, kuna pia Uwezo Fund . Lakini ningependa kushikilia mambo mawili. Kwanza, ni swala sugu la ufisadi. Nilipoangalia hii Ripoti ambayo imeletwa na Tume ya Kupigana na Ufisadi, ni Ripoti ambayo kwa kusema kweli, inashika viongozi wengi katika wale ambao wamechaguliwa kisiasa. Uchunguzi wa ripoti hii haujakamilika. Lakini leo ukitajwa kua wewe ni mfisadi, nakupa mia fil mia; mwananchi aliyekupigia kura anatoka imani. Hili ni suala ambalo linatatiza sana. Niliposikia kuwa kutakuwa na ripoti kuhusu magavana na jinsi wanavyopora fedha za umma, nilidhani kutakuwa na mabilioni ya pesa ambazo zitaonyeshwa kuwa zimepotea. Lakini ripoti hii inazungumzia Ksh140 millioni na Ksh160 millioni. Kupitia ugatuzi, ambao tumeupitisha kikatiba, tunasukuma pesa nyingi sana kwa serikali za kaunti. Hivi sasa, Serikali ya Kitaifa imesukumia serikali za kaunti Ksh258 bilioni. Hizo pesa zinaenda mashinani kupitia kwa kaunti. Katika maeneo mengine, hakuna kazi yoyote iliyofanywa. Pesa nyingi sana zinafujwa, lakini katika ripoti hii, kitu kinachoshangaza ni kwamba hakuna habari ya kisawasawa ya kutuonyesha kuwa kweli pesa zimepotea kivipi. Suala la ufisadi ama suala la dhuluma za kihistoria si kuteswa peke yake; bali pia ni kunyang’anywa mashamba. Ninapozungumza, kwenye sehemu yangu ya uwakilishi bungeni, kuna mahali panapoitwa Kiwambale, ambako kuna wanavijiji ambao wameishi hapo kwa miaka 100. Lakini sasa hivi, wako katika hatari ya kuondolewa. Rais ametamka yeye mwenyewe akasema kwamba hata wale---"
}